Wilaya ya Rungwe ni kati ya wilaya 7 za Mkoa wa Mbeya katika Tanzania na ina Postikodi namba 53500.

Thumb
Mahali pa Rungwe (kijani) katika mkoa wa Mbeya.
Thumb
Daraja la Mungu ni kati ya maajabu asilia ya wilaya hii.

Imepakana na Wilaya ya Mbeya vijijini upande wa kaskazini, Mkoa wa Iringa upande wa mashariki, Wilaya ya Kyela upande wa kusini-mashariki, Wilaya ya Ileje kwa kusini-magharibi na Mbeya Mjini kwa magharibi.

Makao makuu ya wilaya yako Tukuyu.

Jina la wilaya limetokana na kituo cha misheni ya Moravian cha Rungwe kilichopo kwenye mitelemko ya mlima wa Rungwe takriban km 20 kutoka Tukuyu.

Rungwe ni hasa eneo la Wanyakyusa ikishika sehemu kubwa ya eneo la Unyakyusa lililoitwa kihistoria pia "Konde".

Mwaka 2002 wilaya ilikuwa na wakazi 307,270.[1] Katika sensa ya mwaka 2022 walihesabiwa 273,536 [2] baada ya mwaka 2013 kata 11 kutengwa na Rungwe na kuunda Wilaya ya Busokelo.

Barabara kuu kutoka Dar es Salaam - Iringa - Mbeya kwenda Malawi inapita eneo la wilaya.

Rungwe inapokea mvua nyingi na iko kati ya maeneo yenye rutuba sana katika Tanzania.

Kati ya mazao ya sokoni kuna mashamba makubwa ya chai.

Tanbihi

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.