Pepin Mfupi (kwa Kifaransa: Pépin le Bref; 714 hivi – 24 Septemba 768) alikuwa mfalme wa Wafaranki tangu mwaka 751 hadi kifo chake. Ndiye mwanzilishi wa nasaba ya Wakarolo.

Thumb
Mchoro mdogo wa Pipino Mfupi, Anonymi chronica imperatorum, 1112–1114 hivi.

Mtoto wa Karolo Nyundo na mke wake Rotrude wa Hesbaye, alilelewa na wamonaki wa Basilika la Mt. Denis.

Alipomrithi baba yake kama Mkuu wa ikulu mwaka 741, alitawala nchi pamoja na kaka yake Carloman. Pipino alitawala Neustria, Burgundy na Provence, na Carloman alitawala Austrasia, Alemannia na Thuringia. Walikomesha uasi wa Wabavaria, Waakwitania, Wasaksoni na wa Waalemani, halafu mwaka 743 walimtawaza Kilderiki III mfalme wa mwisho wa Wamerovinji.

Wakiheshimu Kanisa na Papa, waliendeleza sera ya baba yao kwa kumuunga mkono Boniface katika kurekebisha Kanisa la Wafaranki na kuinjilisha Wasaksoni.

Baada ya Carloman kutawa mwaka 747, Pipino alimlazimisha Kilderiki kujiunga na monasteri akawa mfalme mwenyewe kwa msaada wa Papa Zakaria mwaka 751.

Alijitahidi kueneza utawala wake, alirekebisha sheria za Wafaranki na alimuunga mkono Papa Stefano II dhidi ya Walombardi nchini Italia. Kwa kumpa Papa miji kadhaa, aliweka msingi wa Dola la Papa.

Aliteka Septimania kutoka kwa Waislamu Umayyad na kupambana na makabila mbalimbali ya Kijerumani.

Alipofariki alirithiwa na wanae Karolo Mkuu na Karlomano I.

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.