Bonifas mfiadini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Bonifas mfiadini

Bonifas (kwa Kilatini Bonifacius, yaani Mtendamema, ambaye aliitwa Wynfrith kabla ya kutajiwa na Papa Gregori II jina hilo jipya; Crediton, Wessex, 673 hivi - Dokkum, 5 Juni 754) alikuwa mmonaki Mbenedikto kutoka Uingereza aliyetumwa kama mmisionari huko Ujerumani (716).

Thumb
Mt. Bonifas akibatiza Wasaksoni na Kifodini cha Mt. Bonifacio, katika Sakramentari ya Fulda (karne XI).
Thumb
Kadi ya karne ya 20 ikimuonyesha Bonifas akihama Uingereza.
Thumb
Kifo cha Mt. Bonifas, kilivyochongwa na Werner Henschel, 1830, Fulda.
Thumb
Kikanisa cha Mt. Bonifas chini ya ardhi, Fulda

Ili kushinda vipingamizi alikwenda huko Roma akafanywa kwanza askofu (722), baadaye askofu mkuu (732), na baadaye tena balozi wa Papa (738), akijitahidi kuimarisha Kanisa katika dola lote.

Hatimaye akawa mfiadini pamoja na wenzake walau 9 katika Uholanzi wa leo.

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na wengineo kama mtakatifu, akiitwa pengine "mtume wa Ujerumani"[1].

Sikukuu yake ni tarehe 5 Juni ya kila mwaka[2].

Sala yake

Mungu wa milele, kimbilio la wanao wote, katika udhaifu wetu ndiwe nguvu yetu, katika giza letu ndiwe mwanga wetu, katika uchungu wetu ndiwe faraja na amani yetu.

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.