Pep Guardiola
kocha na mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu kutoka nchini Hispania From Wikipedia, the free encyclopedia
Josep "Pep" Guardiola Sala, (amezaliwa 18 January 1971 [1]) ni meneja wa soka la kulipwa,Raia wa Uhispania na mchezaji wa mpira wa miguu wa zamani, ambaye ni meneja wa klabu ya Manchester City tangu 2016. Anachukuliwa kuwa mmoja wa wasimamizi muhimu katika historia ya soka. [2] Na anashikilia rekodi za mechi nyingi mfululizo za ligi alizoshinda kwenye La Liga akiwa na klabu ya Barcelona F.C.[3]

Guardiola alikuwa kiungo mkabaji. Alitumia muda mwingi wa maisha yake akiwa na Barcelona,Pia alikuwa sehemu ya timu ya Johan Cruyff iliyoshinda kombe la kwanza la klabu bingwa Ulaya mwaka 1992 [4]. na kushinda makombe manne mfululizo katika ligi kuu ya Uhispania (1991-1994).Alikuwa nahodha wa timu kutoka mwaka 1997 hadi 2001 alipoondoka katika klabu hiyo.Guardiola aliwahi kucheza Brescia na Roma nchini Italia, Al-Ahli ya Qatar, na Dorados de Sinaloa ya Mexico.Alicheza mara 47 akiwa kama nahodha wa timu ya taifa ya Uhispania , na alicheza kwenye Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 1994, na vile vile kwenye UEFA Euro ya mwaka 2000.
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.