From Wikipedia, the free encyclopedia
Papa Innocent I alikuwa Papa kuanzia tarehe 22 Desemba 401 hadi kifo chake tarehe 12 Machi 417[1]. Alitokea Albano, Roma, Italia[2].
Jambo la pekee katika historia ya Kanisa[3], alimfuata Papa Anastasio I, aliyemzaa kabla ya kupewa upadrisho, akafuatwa na Papa Zosimus.
Aliimarisha mamlaka ya Kanisa la Roma kwa kuamua kesi nyingi za pande zote mbili za Kanisa[4], Mashariki na Magharibi[5]. Alimtetea Yohane Krisostomo, alimfariji Jeromu na kumkubali Augustino.
Alieneza[6] kanuni ya vitabu rasmi vya Biblia inayolingana na ile itakayopitishwa na Mtaguso wa Trento miaka elfu baadaye[7][8][9].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.