Papa Anastasio I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Papa Anastasio I

Papa Anastasio I alikuwa Papa kuanzia tarehe 27 Novemba 399 hadi kifo chake tarehe 19 Desemba 401[1]. Alitokea Roma, Italia. Baba yake aliitwa Maximus.

Thumb
Papa Anastasio I.

Alimfuata Papa Siricius akafuatwa na mwanae aliyemzaa kabla hajapadrishwa, Papa Inosenti I, jambo la pekee katika historia ya Kanisa[2].

Mwenye ari kubwa, alilaani mafundisho kadhaa ya Origen na kuhimiza Wakristo wa Afrika Kaskazini wapinge Udonato[3].

Alikuwa rafiki wa Augustino wa Hippo, Jeromu na Paulino wa Nola. Jeromu alimsifu kama mtu mwenye utakatifu mkubwa na tajiri sana katika ufukara wake[4].

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Desemba[5].

Tazama pia

Maandishi yake

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.