From Wikipedia, the free encyclopedia
Nunzio Sulprizio (Pescosansonesco, Pescara, 13 Aprili 1817 – Napoli, 5 Mei 1836) alikuwa mhunzi mwanagenzi wa Italia.[1][2]
Katika maisha yake mafupi kama yatima dhaifu na mwenye ugonjwa wa kudumu mguuni alisifiwa kwa maadili yake. Alistahimili mateso yote kwa utulivu na furaha, akiwahudumia na kuwafariji wagonjwa wengine, na akiwa fukara mwenyewe alijitahidi kusaidia alivyoweza maskini wote.
Papa Paulo VI alimtangaza mwenye heri tarehe 1 Desemba 1963 baada ya miujiza miwili kutokea kwa maombezi yake.[1] Halafu alitangazwa na Papa Fransisko kuwa mtakatifu tarehe 14 Oktoba 2018.
Sikukuu ya Mt. Nunzio inaadhimishwa tarehe 5 Mei, siku ya kifo chake[3].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.