Nikolasi wa Myra (Mtakatifu Nikolasi kwa Kigiriki Ἅγιος Νικόλαος agios nikolaos; 2706 Desemba 343),[1][2] alikuwa askofu wa mji wa Myra akaendelea kuwa mmoja wa watakatifu maarufu zaidi wa Kanisa la Kikristo.

Thumb
Nikolasi wa Myra jinsi alivyochorwa na mtawa Mrusi katika karne ya 12.

Tarehe 6 Desemba ni sikukuu yake[3] inayosheherekewa na Wakristo Wakatoliki, Waorthodoksi na pia na sehemu ya Waprotestanti katika Ulaya ya kati na kaskazini.

Maisha

Hakuna habari nyingi za kihistoria zenye uhakika juu ya maisha yake lakini hadithi zilizosimuliwa juu yake ziko tele.

Myra leo hii inaitwa Demre, ni mji kusini mwa Uturuki, si mbali na Antalya. Ulikuwa mji wa bandari.

Nikolasi alikuwa na sifa ya kutenda miujiza pamoja na uponyaji.

Anasemekana alikuwa na tabia ya kuwaletea watu maskini na watoto zawadi kwa siri; kwa hiyo hukumbukwa hadi leo kwenye sikukuu yake ambako watoto katika nchi mbalimbali hupokea zawadi zinazowekwa ndani ya viatu au ndani ya soksi.

Kutokana na desturi hii amekuwa pia kielelezo au chanzo cha Baba Krismasi iliyo desturi badala ya Nikolasi.

Katika Ulaya ya karne za kati aliheshimiwa kama mtakatifu msimamizi wa wanabahari na wafanyabiashara; hapo ni sababu mojawapo ya kwamba kuna makanisa mengi sana yenye jina lake.

Picha

Tazama pia

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.