Mwangata ni kata ya Manisipaa ya Iringa, Mkoa wa Iringa, Tanzania yenye Postikodi namba 51112.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 24,673 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,486 waishio humo.[2]

Jina Mwangata linasemekana lilitokana na uwepo wa mzee mmoja mtaalamu wa jadi katika eneo hilo. Mzee huyo alikuwa akitoa tiba yake kwa mfumo wa pekee kwani alikuwa akichukua vijiti vidogovidogo pamoja na magome halafu alifunga kama 'ngata' ya kubebea kuni/maji ambayo kwa lugha asilia ya Kihehe inaitwa ng'ata. Hivyo basi wanakijiji walikuwa wakisema kuwa wanakwenda kwa mtaalamu "mwangata" na jina hilo likapata umaarufu mkubwa na mpaka sasa bado linatumika. [3]

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.