From Wikipedia, the free encyclopedia
Miamba mashapo (kwa Kiingereza: sedimentary rocks) hutokea pale ambapo mashapo hukaa kwa muda mrefu yakifunikwa na mashapo mengine na kuathiriwa na uzito wa matabaka ya juu yanayosababisha shinikizo kubwa. Miamba ya aina hiyo hufanya sehemu kubwa ya uso wa ardhi, ingawa Dunia kwa jumla kuna zaidi miamba ya mgando (igneous rocks) na miamba metamofia (metamorphic rocks).
Mashapo kwa kawaida ni mata inayokusanyika chini kwenye mito, maziwa na bahari baada ya kupelekwa huko na mwendo wa maji, kiasi pia kwa mwendo wa upepo. Mata ya mashapo ni pamoja na vipande vidogo vya mawe yaliyosagwa au kuvunjikavuunjika, mabaki ya mimea au wanyama na mata yaliyotokana na utendanaji wa kikemia.
Miamba mashapo inapatikana hasa ya aina tatu: gange (mawe ya chokaa, limestone), jiwe mchanga (sandstone) na mwambatope (shale). [1]
Miamba mashapo hufunika asilimia 75 – 80 za uso wa ardhi, lakini hufanya 5% tu za ganda la Dunia. Viwango husianifu wa aina za miamba mashapo ni kama ifuatavyo:
Kama mashapo yameshinikizwa kwa nguvu ya kutosha kwa muda mrefu, huimarishwa na kugeuka kuwa mwamba thabiti. Iliyopandwa na kushinikizwa kwa muda, matope huwa 'yameunganishwa' (yamefanywa kuwa thabiti) kuwa safu ya mwamba. Katika mwamba huo matabaka yanatambulika yanayoonyesha jinsi gani mashapo yalivyojipanga wakati wa kushuka kwenye tako la bahari na kufunikwa na matabaka mapya.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.