Mto Salawin
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mto Salawin (kwa Kiingereza: Salween) ni mto mkubwa katika Asia ya Kusini-Mashariki. Chanzo chake kipo Tibet (China) halafu unapita Myanmar na Uthai kwenye mwendo wake wa takriban kilomita 2,400[1].
Majina yake hutofautiana kadiri ya nchi ambako unapita: Watibet huuita Nag Qu, pale China huitwa 怒江 Nù Jiāng, pale Myanmar Thanlwin Myit (pamoja na majina mengine) na mwishoni katika Uthai Maenam Salawin (แม่น้ำสาละวิน).
Mto huo unatokea kwenye Nyanda za Juu za Tibet na kuelekea magharibi mwanzoni. Lakini baadaye unageuka mashariki na kusini ukiishia katika Bahari ya Andamani huko Mawlamyaing, Myanmar.
Kwa njia ya kilomita 120 hivi mto huu ni mpaka baina ya Uthai na Myanmar, sehemu yake ya mwisho kabla ya bahari unarudi tena ndani ya Myanmar.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.