Ruaha Mkuu
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ruaha Mkuu (pia: Ruaha Mkubwa) ni mto muhimu nchini Tanzania na tawimto la Rufiji. Huitwa "Ruaha Mkuu" kwa kuutofautisha na "Ruaha Mdogo" unaoishia ndani yake, si mbali na Iringa Mjini.
Chanzo chake ni mito mingi midogo inayotelemka milima ya nyanda za juu za kusini mwa Tanzania, hasa safu za milima ya Uporoto na ya Kipengere. Mito hii inakusanya maji yake kwenye tambarare ya Usangu na ndipo Ruaha inapoanza. Mito mikubwa zaidi inayoungana hapa na kuunda Ruaha ni pamoja na mto Mbarali, mto Kimani na mto Chimala.
Karibu na Ng’iriama mto unatoka katika Usangu na kuingia hifadhi ya kitaifa ya Ruaha. Inaendelea kupokea Ruaha Mdogo na mto Kisigo kabla ya kuingia katika ziwa la lambo la Mtera, halafu inaendelea hadi lambo la Kidatu.
Baada ya Kidatu, Ruaha Mkuu unapita tambarare ya Kilombero hadi kuishia katika mto Rufiji.
Maji ya Ruaha Mkuu ni muhimu kwa ekolojia ya beseni lake pamoja na watu wote wanaoishi huko. Lakini matumizi ya binadamu yameleta mvurugo kwa ekolojia ya mto na tangu mwaka 1993 mto umeanza kukauka wakati wa ukame. Uhaba wa maji umesababishwa na matumizi mabaya ya maji upande wa miradi mikubwa ya mpunga katika Usangu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.