From Wikipedia, the free encyclopedia
Mtakatifu Mauro, O.S.B. (Roma, Italia, 512 - Glanfeuil, Ufaransa, 584) alikuwa mfuasi mpenzi wa Benedikto wa Nursia, kama inavyoelezwa na Gregori Mkuu katika masimulizi manne juu yake ambayo yalitumika sana baadaye katika malezi ya Wabenedikto[1].
Humo tunasikia kwamba wazazi wake walikuwa wa koo bora za Roma wakamtoa bado mtoto monasterini ili afuate maisha ya kitawa.
Baadaye alijitokeza kwa utiifu wake kwa abati wake na hata kwa miujiza mbalimbali.
Mauro alikuwa mwandamizi wa kwanza wa Benedikto kama abati wa Subiaco[2].
Habari nyingi zaidi zilitungwa katika karne ya 9 lakini si za kuaminika.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu tarehe 15 Januari, au, pamoja na mwenzake Plasido, tarehe 5 Oktoba.[3]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.