From Wikipedia, the free encyclopedia
Milima ya Nuba (kwa Kiarabu جبال النوبة jabal an-nuba) ni eneo lililo katika Kordofan Kusini, Sudan. Eneo hilo ni nyumbani kwa kundi la makabila ya asili yanayojulikana kwa pamoja kama Wanuba.
Katika karne ya 18 eneno lilikuwa chini ya wafalme wa Wanuba waliojulikana kama Taqali, walioshindwa na Dola la Mahdi. Wakati ule wahamiaji Waarabu wengi Wabaggara waliingia katika maeneo ya Kordofan Kusini.
Hadi sasa watu milioni 1.5 wanaishi katika milima hiyo, hasa kabila la Nuba na wachache wa Wabaggara. [1]
Milima inaenea kilomita 64 kwa 145 ikifikia kimo cha mita 450 hadi 900 juu ya UB.[2] Tabianchi ni ya kitropiki, joto na nusu-yabisi inayopokea kwa wastani milimita 300 hadi 800 za mvua kwa mwaka. Wakati wa kiangazi kinachoendelea kuanzia Februari hadi Mei mara nyingi kuna uhaba wa maji. [3]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.