From Wikipedia, the free encyclopedia
Memphis ilikuwa mji mkuu wa Misri ya Kaskazini, na baadaye pia ya Misri ya Kale yote kuanzia maungano ya Misri ya Kaskazini na Misri ya Kusini chini ya Farao Menes hadi karibu mwaka 2200 KK. Baadaye ilirudi tena kama mji mkuu wakati wa Ufalme Mpya wa Misri. [1] Kilikuwa kitovu cha utawala hadi utawala wa Kiroma juu ya Misri.[2] [3]
Jina lake la zamani kwa Kimisri lilikuwa Ineb Hedj ("Kuta Nyeupe"). Jina "Memphis" ( Μέμφις ) lilitungwa na Wagiriki waliojaribu kutamka jina la piramidi ya Pepi I (nasaba ya 6), ambayo ilikuwa Men-nefer, [4] likawa Menfe katika matamshi ya kawaida.
Miji ya kisasa ya Mit Rahina, Dahshur, Saqqara, Abusir, Abu Gorab, na Zawyet el'Aryan, kusini mwa Kairo, yote iko ndani ya mipaka ya kiutawala ya Memphis ya kihistoria ( 29°50′58.8″N, 31°15′15.4″E ).
Memphis pia ilijulikana katika Misri ya Kale kama Ankh Tawy ("Inayoshika nchi zote mbili") kwa sababu ya nafasi ya kimkakati ya mji kati ya Misri ya kusini na Misri ya kaskazini.
Maghofu ya Memphis yako km 20 kusini mwa Kairo, kwenye ukingo wa magharibi wa mto Nile.
Katika Biblia, Memphis inaitwa Moph au Noph.
Maghofu yake pamoja na maeneo mapana ya makaburi ya enzi za Misri ya Kale, pamoja na Sakara na Pirmidi za Gizeh, yamepokelewa katika orodha ya Urithi wa Dunia ya UNESCO[5].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.