Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mdororo Mkuu ulikuwa kipindi ambacho uchumi wa Marekani na sehemu nyingine za dunia ulikuwa mbaya sana. Ulianza na Kuanguka kwa Soko la Hisa la Marekani 1929. Bei za masoko katika Soko la Hisa la Marekani zilianguka kuanzia tarehe 24 Oktoba hadi 29 Oktoba 1929. Watu wengi sana walipoteza kazi zao. Watu wengi wakawa maskini na kutokuwa na makazi. Hii ilimaliza utajiri wa Roaring Twenties. Ile siku ambayo imesemwa kuwa mwanzo wa Mdororo Mkuu inaitwa "Black Tuesday."
Wakati Mdororo Mkuu umeanza, Herbert Hoover ndiye aliyekuwa rais wa Marekani. Watu walipiga kura kwa ajili ya rais mpya hapo 1932. Jina lake lilikuwa Franklin D. Roosevelt. Roosevelt alivyopata serikali akapata kupitisha sheria mpya na mipango ya kusaidia watu ambao walipata kuumizwa na Mdororo Mkuu. Hiyo mipango ilikuwa inaitwa New Deal.
Mdororo Mkuu ulikuwa mbaya sana, lakini kwa msaada wa kila mmoja, kukawa na afadhali, na kila kitu kikaja kuwa sawa. Kati ya miaka 1939 na 1944 watu wengi wakapata kazi tena kwa sababu ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, na huo Mdororo Mkuu ukawa unaelekea ukingoni na maisha yakawa kawaida na si kama hapo awali.
Nchi | Kiasi cha kupungukiwa |
---|---|
Marekani | − 46,8 % |
Poland | − 46,6 % |
Kanada | − 42,4 % |
Ujerumani | − 41,8 % |
Chekoslovakia | − 40,4 % |
Uholanzi | − 37,4 % |
Italia | − 33,0 % |
Ufaransa | − 31,3 % |
Ubelgiji | − 30,6 % |
Argentina | − 17,0 % |
Denmark | − 16,5 % |
Ufalme wa Maungano (Uingereza) | − 16,2 % |
Uswidi | − 10,3 % |
Japani | − 8,5 % |
Brazil | − 7,0 % |
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdororo Mkuu kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mdororo Mkuu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.