Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo wa Tanzania From Wikipedia, the free encyclopedia
Mbwana Yusuph Kilungi (anajulikana kwa jina lake la kisanii kama Mbosso; amezaliwa 3 Oktoba 1991) ni mwimbaji, mtunzi na mwanamuziki kutoka nchini Tanzania.
Umaarufu ulianza akiwa na kundi zima la Yamoto Band ambalo ndani yake kuliwa na Aslay, Beka Flavour, Enock Bella na Mbosso. Kwa pamoja walikuwa wanaunda Yamoto Band chini ya Mkubwa Fella na Wanawe. Jina la Mkubwa na Wanawe lilikuwa na hadi sasa bado lipo hivyo hivyo kama Mkubwa na Wanawe. Ndani ya mkubwa na Wanawe kuna vipaji mbalimbali.
Baada ya Yamoto Band kufa, Mbosso aliamua kurudi nyumbani kwao kijijini huko Kibiti. Ambapo alijihusisha na vitendo mbalimbali vya kihalifu hasa kwa kukata tamaa na kuona wenzi wake wakiwa wanapata mafanikio yeye akiwa amebaki tu nyumbani. Jambo hili, lilikuwa tofauti kidogo na kina Aslay na Beka Flavour. Hawa waliendelea kutamba katika muziki hadi hapo Diamond Platnumz alipoona muda huu unafaa sasa kumrudisha Mbosso katika tasnia ya muziki kama alivyomuahidi mnamo mwakwa 2014 ya kwamba atamsaidia na kumuweka kwenye ramani ya muziki wa Bongo Flava. Wimbo wa kwanza wa Mbosso ulitoka mnamo tarehe 28 Januari 2018 na ulikwenda kwa jina la Watakubali.[1]
29 Januari alitambulishwa mbele ya hadhira ya kwamba yeye ni msanii kamili aliyesaini mkataba na WCB.[2]
Hadi sasa Mbosso ametoa wimbo kama vile Watakubali, Nimekuzoea, Alele, Shida, Picha Yake, Hodari, Nipepe, Hodari, Tamu. Wimbo mwingine aliotoa na kundi la Wasafi jina lake lilikuwa Zilipendwa na wimbo mwingine aliotoa na Diamond Platnumz na lavalava wimbo ambao jina lake ni Jibebe.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.