From Wikipedia, the free encyclopedia
Marcia Anne Cross (alizaliwa 25 Machi 1962) ni mwigizaji wa Marekani. Anajulikana katika uigizaji kama mhusika wa Bree Van de Kamp kwenye kipindi cha Desperate Housewives.
Marcia Cross alisoma shule ya msingi na ya upili katika shule ya Juilliard mjini New York, na kisha akafuzu kwa shahada ya pili ya saikolojia kutoka kwa chuo kikuu cha Antioch mjini Los Angeles. Alianza kuigiza mnamo 1984 kwenye kipindi cha The Edge of Night. Baadaye, aligura kutoka mji wa New York hadi Los Angeles na kisha akaigiza kwenye filamu ya The Last Days of Frank and Jessie James. Kuanzia 1986 hadi 1987, aliigiza kama Kate Sanders kwenye kipindi cha One Life to Live.
Mnamo 1992, Cross aliigiza kama Dkt. Kimberley Shaw kwenye kipindi cha Melrose Place. Hapo awali, alikuwa amepewa mkataba wa kuigiza kwenye kipindi hiki kwa muda wa msimu mmoja, lakini aliwafurahisha watayarishaji wakuu hadi wakakubali kumweka mpaka msimu wa nne.
Baada ya kuwacha Melrose Place, Cross alijiunga na kipindi cha Seinfield ambapo aliigiza kama Dkt. Sitarides. Pia, ameigiza kwenye vipindi kama CSI: Crime Scene Investigation, Profiler, Everwood na Touched by an Angel.
Mnamo 2004, Cross alifaulu kujiunga na kipindi cha Desperate Housewives.
Cross alizaliwa mjini Marlborough, Massachusetts. Yeye alikuwa rafiki wa dhati wa Richard Jordan. Jordan alikuwa mkubwa wa Cross kwa miaka ishirini na tano. Yeye alikufa kutokana na uvimbe wa ubongo mnamo 1993.
Cross aliolewa na Tom Mahoney mnamo 24 Juni 2006.[1] Mnamo 6 Septemba 2006, alitangaza kuwa yeye ni mjamzito. Mnamo 20 Februari 2007 Cross alijifungua pacha: Eden na Savannah katika hospitali mjini Los Angeles.[2]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.