Kozi ni ndege mbuai wadogo wa familia ya Falconidae.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Kozi |
Kozi tembere |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Falconiformes (Ndege kama kozi)
|
Familia: |
Falconidae (Ndege walio na mnasaba na kozi) Leach, 1820 |
|
Ngazi za chini |
Nusufamilia 3, jenasi 11:
- Caracarinae D'Orbigny, 1837
- Caracara Merrem, 1826
- Daptrius Vieillot, 1816
- Ibycter Vieillot, 1816
- Milvago Spix, 1824
- Phalcoboenus Orbigny, 1834
- Spiziapteryx Kaup, 1852
- Falconinae Leach, 1820
- Herpetotherinae Lesson, 1843
- Herpetotheres Vieillot, 1817
- Micrastur G.R. Gray, 1841
|
Funga
Wana mabawa membamba yaliyochongoka ambayo yanawapa uepesi na uwezo wa kubadilisha mwelekeo upesi. Kozi tembere, ndege wepesi kabisa duniani, wanaweza kufikia kasi ya kushuka ya zaidi ya km 300 kwa saa.
Kozi hula mawindo madogo kama ndege, panya, mijusi na wadudu. Spishi nyingine hutumika sana kwa uwindaji kwa ndege mbuai.
Jike hutaga mayai juu ya miamba, ndani ya mianya, juu ya tawi kubwa au ndani ya tago la ndege mwingine kama kunguru. Mara nyingi hawatumii vijiti au vitu vingine kujenga tago salihi.
- Falco alopex, Kozi Mwekundu (Fox Kestrel)
- Falco amurensis, Kozi wa Amur (Amur Falcon)
- Falco araeus, Kozi wa Shelisheli (Seychelles Kestrel)
- Falco ardosiaceus, Kozi Kijivu (Grey Kestrel)
- Falco biarmicus, Kozi Marumbi (Lanner Falcon)
- Falco cherrug, Kozi Madoa (Saker Falcon)
- Falco chicquera, Kozi Kisogo-chekundu (Red-necked Falcon)
- Falco columbarius, Kozi Njiwa (Merlin)
- Falco concolor, Kozi Mweusi (Sooty Falcon)
- Falco cuvierii, Kozi Mlake (African Hobby)
- Falco dickinsoni, Kozi Kiuno-cheupe (Dickinson's Kestrel)
- Falco duboisi, Kozi wa Reunion (Réunion Falcon) imekwisha sasa
- Falco eleonorae, Kozi wa Eleonora (Eleonora's Falcon)
- Falco fasciinucha, Kozi wa Taita (Taita Falcon)
- Falco naumanni, Kozi Mdogo (Lesser Kestrel)
- Falco newtoni, Kozi wa Madagaska (Malagasy Kestrel)
- Falco pelegrinoides, Kozi-jangwa (Barbary Falcon) - labda nususpishi ya F. peregrinus
- Falco peregrinus, Kozi Tembere (Peregrine Falcon)
- Falco punctatus, Kozi wa Morisi (Mauritius Kestrel)
- Falco rupicoloides, Kozi Macho-meupe (Greater Kestrel)
- Falco rupicolus, Kozi-miamba (Rock Kestrel)
- Falco subbuteo, Kozi wa Ulaya (Eurasian Hobby)
- Falco tinnunculus, Kozi Kichwa-kijivu (Common Kestrel)
- Falco vespertinus, Kozi Miguu-myekundu (Red-footed Falcon)
- Falco zoniventris, Kozi Tumbo-miraba (Banded Kestrel)
- Polihierax semitorquatus, Kozi Kibete (African Pygmy Falcon)
Kozi wa Amur
Kozi wa Shelisheli
Kozi kijivu
Kozi marumbi
Kozi madoa
Kozi kisogo-chekundu
Kozi njiwa
Kozi mweusi
Kozi mlake
Kozi kiuno-cheupe
Kozi wa Eleonora
Kozi wa Taita
Kozi mdogo
Kozi wa Madagaska
Kozi-jangwa
Kozi tembere
Kozi wa Morisi
Kozi macho-meupe
Kozi-miamba
Kozi wa Ulaya
Kozi kichwa-kijivu
Kozi miguu-myekundu
Kozi kibete