Klotilda malkia
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Klotilda malkia (pia: Chrotechildis, Chrodigilde au Rotilde; Lyon, Ufaransa 475 - Tours, Ufaransa, 3 Juni 545[1]) alikuwa mtoto wa Kilperiko II, mfalme wa Burgundy, halafu mke wa Klovis I, mfalme wa Wafaranki, ambao wazao wake wakaja kutawala kwa miaka zaidi ya 200[2][3].
Tangu alipoolewa (493) alijitahidi kumvuta mumewe kwenye Ukristo[4] hadi akafaulu kwa sala zake kumfanya abatizwe (496). Tukio hilo likawa na matokeo makubwa kwa historia ya Kanisa na ya Ulaya nzima, kwa kuwa kabila lote lilimfuata kuingia Kanisa Katoliki bila kupitia Uario uliowahi kufuatwa na makabila mengine ya Kijerumani[5]. Ushirikiano wa Wafaranki na Mapapa ukaandaa mwanzo wa Dola Takatifu la Kirumi wakati wa Karolo Mkuu.
Baada ya kufiwa mumewe alikwenda kuishi monasterini asitazamwe tena kama malkia, bali tu kama mtumishi wa Bwana, pamoja na kusaidia maskini na kujenga makanisa[6][7].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[8].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.