From Wikipedia, the free encyclopedia
Klemens Maria Hofbauer (Tasovice, Moravia, leo nchini Ucheki, 26 Desemba 1751 - Vienna, Austria, 15 Machi 1820) alikuwa mtawa na padri wa shirika la Mkombozi Mtakatifu sana, ambaye anajulikana kwa kulieneza nje ya Italia na kufanya utume mkubwa sana[1].
Alijitahidi kwa namna ya ajabu kueneza imani katika nchi za mbali na kuyahuisha maisha ya Kanisa. Akiwa na akili na maadili ya hali ya juu, alivuta wanasayansi na wasanii wengi kwa Kanisa Katoliki.
Alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri tarehe 29 Januari 1888, halafu Papa Pius X alimtangaza mtakatifu tarehe 20 Mei 1909.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.