From Wikipedia, the free encyclopedia
Kitongoji duni (pia: mtaa wa vibanda; kwa Kiingereza slum) ni mtaa jijini ambao mara nyingi huwa na nyumba duni zilizosimikwa karibu, miundomsingi duni na wakazi maskini.
Huduma za usambazaji wa maji safi, umeme na usalama huwa adimu. Vitongoji duni mara nyingi hupatikana mijini katika nchi zinazokua kimaendeleo kwa sababu ya kiwango kikuu cha ukuaji na uhamiaji.[1]
Vitongoji duni huanzia pambizoni mwa miji karibu au katika ardhi ambazo hazina thamani kubwa, ni za serikali au milki ya ufadhili au taasisi ya dini au hazina hatimiliki hakika.[2] Baadhi ya vitongoji duni hujipa majina ya vyama vya kisiasa, watu tajika kihistoria, wanasiasa ama watu waliokuwa wamiliki wa ardhi hiyo. Kwa mfano, vitongoji duni Mukuru kwa Njenga na Mukuru kwa Ruben.
Baadhi ya wahamiaji huchukulia ardhi ambayo haina wakazi kuwa haina wamiliki na hivyo basi wakapakaa.[3]Serikali pia inaweza kugawia watu ploti na baadaye ardhi hiyo ikabadilika kuwa kitongoji duni na watu kupoteza haki ya kudai ploti. Kwa mfano, Kibera.[4]
Vitongoji duni huwa na vyumba duni. Mara nyingi, ubora wa vyumba hauwezi kustahimili mvua nyingi au upepo mkali. Vifaa vya ujenzi huwa karatasi, plastiki n.k. Sakafu za mchanga, kuta za matope, mbao zilizoshikiliwa kwa kamba, au mabati. Hata wakati nyumba zimejengwa kwa mawe na simiti, hakuna umakinifu katika muundo na uhandisi wa jengo na hivyo basi, majengo hayo hayazingatii kanuni za serikali za ujenzi.[5] Nyumba hizo pia huwa zimejengwa karibu sana.
Vitongoji duni huwa havina miundomsingi ya kutosha. Kama vile, maji safi, umeme, huduma za afya, usalama na polisi, usafiri wa umma, huduma za zimamoto, ambulensi, mfumo wa majitaka na barabara sakifu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.