Juliani wa Toledo (Toledo, Hispania, 642 - Toledo, 690) alikuwa mmonaki mwanateolojia aliyehudumia kama askofu mkuu wa Toledo na kuacha kumbukumbu ya umakini katika haki, upendo na juhudi kwa ajili ya wokovu wa watu.
Aliunganisha Kanisa la rasi ya Iberia na kuendesha sinodi na mitaguso mbalimbali pamoja na kurekebisha liturujia ya Toledo. Pia aliandika sana juu ya mambo mbalimbali akithibitisha imani sahihi.
Tangu zamani anaheshimiwa kama mtakatifu.
Tazama pia
Tanbihi
Vyanzo
Maandishi yake
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.