Remove ads
From Wikipedia, the free encyclopedia
Mwanateolojia ni mtu anayeshughulikia teolojia au ujuzi juu ya habari za Mungu kitaalamu. Ni tofauti na mtaalamu wa dini anayeweza kuchungulia dini yoyote, kwa sababu mwanateolojia ana msimamo katika mapokeo ya dini moja hasa.
Si lazima awe mwalimu wa dini yake anayetambuliwa na waumini, kwa sababu kitambulisho ni kiwango chake cha elimu si imani. Hata hivyo kuna pia wanateolojia ambao mara nyingi ni viongozi wa kiroho.
Katika mapokeo ya Ukristo wa magharibi mwanateolojia amepita ngazi za chuo kikuu na masomo yake katika idara ya teolojia. Nje ya Ukristo wa magharibi kwa mfano katika Uislamu, Uyahudi na Ukristo wa mashariki kuna pia njia mbalimbali za kukubaliwa kufika kwenye kiwango cha utaalamu wa habari za Mungu.
Katika muundo wa teolojia ya magharibi mwanateolojia ataweka mkazo wake katika masomo ya teolojia kama vile:
na mengineyo.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.