Jiji la Zanzibar ni mji mkubwa wa kisiwa cha Unguja na mji mkuu wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.
Jiji la Zanzibar | |
Mahali pa mji wa Zanzibar katika Tanzania |
|
Majiranukta: 6°9′36″S 39°12′0″E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Unguja Mjini Magharibi |
Wilaya | Unguja Mjini |
Pia ni wilaya katika Mkoa wa Unguja Mjini Magharibi wa Tanzania.
Jina
- Makala kuu: Etimolojia ya Neno Zanzibar
Mji Mkongwe
Kitovu cha historia yake ni Mji Mkongwe (Stone Town) ulioandikishwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (World Heritage).
Nyumba za Mji Mkongwe zilijengwa tangu mwaka 1830 wakati Sultani Sayyid Said alipohamisha mji mkuu wake kutoka Omani kuja Unguja.
Kati ya majengo maarufu ni Beit al Ajaib (yaani Jumba la Maajabu lililobomoka tarehe 24 Desemba 2020[2]), boma la kale, Kanisa Kuu la Kianglikana lililojengwa mahali pa soko la watumwa na hasa nyumba nyingi za kihistoria za ghorofa zilizojengwa na famila za tabaka la matajiri Waarabu zenye milango yenye mapambo mazuri.
Mji Mkongwe unapokea watalii wengi kila mwaka.
Mji wa kisasa umekua sana ng'ambo ya Mji Mkongwe.
Tazama Pia
Picha
- Nyumba ya Maajabu (Beit-al-Ajaib
- Boma la Kale katika Mji Mkongwe
- Mahalipa kuogelea ufukoni karibu na Mji Mkongwe
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand in your browser!
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.