From Wikipedia, the free encyclopedia
Ignasi wa Konstantinopoli (Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 798 hivi – Konstantinopoli, 23 Oktoba 877) alikuwa Patriarki wa Konstantinopoli miaka 847-858 halafu 867-877.
Kisha kuchafuliwa sana jina lake na kaisari Barda, ambaye alikuwa amemlaumu kwa kumtaliki mke wake, alipelekwa uhamishoni, lakini Papa Nikola I akamrudisha hata akaweza kufariki madarakani kwa amani[1].
Farakano la muda kati ya Kanisa la Roma na lile la Konstantinopoli, lililotokea katikati (miaka 863-867) kuhusu upatriarki wake na ule wa mshindani wake, Fosyo, lilikuwa baya kuliko yote kabla ya farakano la mwaka 1054 ambalo limedumu hadi leo kati ya Ukristo wa Magharibi na Waorthodoksi.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu; ajabu zaidi ni kwamba alitangazwa rasmi na Fosyo mwenyewe mwaka 878.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.