From Wikipedia, the free encyclopedia
Gangsta rap au gangster rap [1] ni aina ya muziki wa hip hop ambayo mashairi yake yanahusisha utamaduni wa magenge ya mitaani ya Marekani[2] , iliibuka miaka ya 1980. Baadhi ya wanamuziki wa rap ya mtindo huu hujivunia uhusiano na magenge halisi ya mitaani, kama vile Crips na Bloods. [3] [4]
Waanzilishi wa Gangsta rap ni pamoja na Schoolly D wa Philadelphia mwaka 1985, Ice-T wa Los Angeles mwaka 1986, na N.W.A mwaka 1988. Mnamo 1993, kupitia mtayarishaji wa muziki Dr. Dre, rapa Snoop Dogg, na mtindo wao wa G-funk, muziki wa gangsta rap ulipata umaarufu zaidi.
Gangsta rap imekuwa ikishutumiwa mara kwa mara kwa kuendeleza mienendo isiyofaa na uhalifu, hasa mashambulizi, mauaji, uuzaji wa dawa za kulevya na uasherati.[5] Gangstar rap imekuwa ikikosolewa na baadhi ya watu mashuhuri, akiwemo Spike Lee[6] , mchungaji Calvin Butts na mwanaharakati C. Delores Tucker, hata hivyo watetezi wa Gangsta rap wanabainisha kuwa ni taswira za kisanii sio uidhinishaji wa maisha ya magenge ya mitaani nchini Marekani, na kusema kuwa baadhi ya mashairi huonyesha kupinga ukandamizaji wa kijamii au ukatili wa polisi, na mara nyingi wamewashutumu wakosoaji kuwa na unafiki na upendeleo wa rangi.[7][8]
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.