From Wikipedia, the free encyclopedia
Fransisko Saveri Maria Bianchi (kwa Kiitalia: Francesco Saverio Maria Bianchi; Arpino, Lazio, 2 Desemba 1743 - Napoli, Campania, 31 Januari 1815) alikuwa padri na mtawa wa shirika la Makleri wa Mt. Paulo, maarufu kama Wabarnaba nchini Italia.
Alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri tarehe 22 Februari 1893, tena mtakatifu na Papa Pius XII tarehe 21 Oktoba 1951.
Alijulikana kwa elimu yake, lakini hasa kwa juhudi zake kwa wanafunzi aliokuwanao na kwa maskini wa mji wa Napoli, hata akaitwa "Mtume wa Napoli"[2][3]. Mwenye karama za pekee, alivutia wengi kufuata kama yeye neema ya Mungu.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.