From Wikipedia, the free encyclopedia
Flora na Maria (walifariki Cordoba, leo nchini Hispania, 851) walikuwa Wakristo waliofia imani yao chini ya utawala wa Waislamu[1].
Flora alikuwa na baba Mwislamu na mama Mkristo, kumbe Maria kinyume chake alikuwa na baba Mkristo na mama Mwislamu ambaye alibatizwa muda mfupi baada ya kuolewa. Walipokutana waliamua kujitosa kupinga Uislamu hadharani hata wakafungwa gerezani alipokuwapo askofu Eulogi wa Cordoba. Kisha kuhojiwa na kushawishwa na kadhi wakakatwa kichwa [2][3][4].
Askofu huyo ndiye aliyeandika habari zao [5].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu mabikira wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 24 Novemba [6][7].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.