Mwanafizikia wa Kiitaliano-Amerika From Wikipedia, the free encyclopedia
Enrico Fermi (Roma, Italia, 29 Septemba 1901 – Chicago, Marekani, 28 Novemba 1954) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Italia. Baadaye alihamia Marekani akawa raia wa huko. Hasa anajulikana kwa uchunguzi wake wa atomu na mambo ya kinyuklia kwa jumla. Mwaka wa 1938 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.
'
Enrico Fermi | |
---|---|
Enrico Fermi, 1940s | |
Amezaliwa | 29 Septemba 1901 |
Amefariki | 28 Novemba 1954 |
Kazi yake | mwanafizikia kutoka nchi ya Italia |
Wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, Fermi alikuwa mmoja wa viongozi wa Mradi wa Manhattan huko Marekani, ambao ulifanikisha kubuni na kutengeneza bomu la nyuklia. Fermi aliongoza majaribio ya kwanza ya kutoa nguvu ya nyuklia kwa utaratibu wa kudhibitiwa, na hivyo kuonyesha uwezekano wa kutengeneza bomu la nyuklia.
Baada ya vita, Fermi aliendelea kufundisha na kufanya kazi nchini Marekani, na alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa taasisi ya utafiti wa nyuklia huko Chicago, inayojulikana kama Enrico Fermi Institute. Mchango wake katika sayansi ya nyuklia na fizikia unaheshimiwa kwa kiasi kikubwa, na njia ya kudhibiti nguvu ya nyuklia iliyobuniwa na Fermi imekuwa msingi wa matumizi ya nishati ya nyuklia.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Enrico Fermi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.