Djibloho
From Wikipedia, the free encyclopedia
Djibloho (jina rasmi Jiji la Kiutawala la Djibloho; kwa Kihispania: Ciudad administrativa de Djibloho) [1] ndio mkoa mpya zaidi wa Guinea ya Ikweta.

Ulitengwa katika maeneo ya mkoa wa Wele-Nzas kwa sheria ya mwaka wa 2017.[2] Kusudi la kuuanzisha mkoa huo lilikuwa kuunda mji mkuu mpya wa taifa utakaochukua nafasi ya Malabo iliyopo kwenye kisiwa cha Bioko.
Utawala
Djibloho inajumuisha wilaya mbili za mijini, Ciudad de la Paz na Mbere. Mji mkuu ni Ciudad de la Paz ("Mji wa Amani"), [3] uliojulikana kama Oyala hadi 2017. [4]
Katika uchaguzi wa bunge wa kitaifa wa 2017, Djibloho ilichagua seneta mmoja na mbunge mmoja. [5]
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.