Beseni la Columbia (kwa Kiingereza: Columbia Plateau au Columbia Basin) ni eneo maalum la kijiolojia na kijiografia kaskazini-magharibi mwa Marekani, likiwa katika majimbo ya Marekani ya Washington, Oregon, na Idaho. Ni eneo kubwa lililotokana na mkondo wa mwamba wa gumawesi (basalt) ulioenea kati ya milima ya Cascades na Milima ya Rocky Mountains katika kipindi cha milipuko ya volkeno iliyopandisha magma kutoka koti la Dunia ambayo iliganda kwenye uso wa ardhi. Mto Columbia unatiririka katika eneo hilo.

Thumb
Beseni la Columbia linashika sehemu kubwa ya Mto wa Basalt ya Columbia, iliyoonyeshwa kwa kijani kwenye ramani hii. Miji ya jimbo la Washington ya Spokane, Yakima na Pasco, na jiji la jimbo la Oregon la Pendleton, viko kwenye Beseni la Columbia.

Jiolojia

Takriban miaka milioni 16 hadi 5 iliyopita volkeno zilimwaga kutoka chini kiasi kikubwa cha lava kilichoenea katika kilomita za mraba 160,000 na kuganda kwa unene wa kilomita 1.8.[1]

Wakati mwamba kiowevu ulipanda juu, uso wa ardhi ulishuka polepole katika nafasi iliyotokea chini yake.

Kwa njia hiyo lilitokea beseni la mto Columbia lenye miinuko kati ya mita 60 hadi 1,500 juu ya u.b.[1]

Tabianchi na uoto

Tabianchi ni nusu yabisi na uoto asilia ni hasa vichaka na nyasi [2].

Jiografia

Miji ya jimbo la Washington katika Beseni la Colombia ni pamoja na:

  • Davenport
  • Reardan
  • Kennewick
  • Moses Lake
  • Pasco
  • Pullman
  • Richland
  • Spokane
  • Walla Walla
  • Yakima
  • Goldendale
  • Deer Park

Miji ya Jimbo la Oregon katika Beseni la Columbia ni pamoja na:

  • Hermiston
  • Hood River
  • Pendleton
  • The Dalles
  • Milton-Freewater

Marejeo

Viungo vya nje

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.