Chozi ni ndege wadogo wa familia Nectariniidae. Spishi za jenasi kadhaa zinaitwa neli. Spishi nyingi sana zina rangi kali zinazong'aa juani kama metali. Manyoya ya kati ya mkia ni marefu sana katika spishi nyingine. Domo lao limepindika na hutumika kwa kutoa mbochi katika maua au wadudu katika matundu. Hula mbochi hasa na pengine maji ya matunda na wadudu pia. Wawindaji-buibui, ambao wamo pia katika familia hii, hula wadudu zaidi kuliko chozi.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Chozi |
Chozi tumbo-njano |
Uainishaji wa kisayansi |
Himaya: |
Animalia (Wanyama)
|
Faila: |
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
|
Nusufaila: |
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
|
Ngeli: |
Aves (Ndege)
|
Oda: |
Passeriformes (Ndege kama shomoro)
|
Familia ya juu: |
Passeroidea
|
Familia: |
Nectariniidae (Ndege walio na mnasaba na chozi) Vigors, 1825 |
|
Ngazi za chini |
Jenasi 16:
- Aethopyga Cabanis, 1850
- Anabathmis Reichenow, 1905
- Anthobaphes Cabanis, 1850
- Anthreptes Swainson, 1832
- Arachnothera Temminck, 1826
- Chalcomitra Reichenbach, 1853
- Chalcoparia Cabanis, 1850
- Cinnyris Cuvier, 1816
- Cyanomitra Reichenbach, 1853
- Deleornis Wolters, 1977
- Drepanorhynchus Fischer & Reichenow, 1884
- Dreptes Reichenow, 1914
- Hedydipna Cabanis, 1850
- Hypogramma Reichenbach, 1853
- Leptocoma Cabanis, 1850
- Nectarinia Illiger, 1811
|
Funga
Ndege hawa wanatokea kanda za tropiki na nusutropiki za Afrika, Asia na kaskazini mwa Australia. Tundu lao lina umbo la mfuko na limening'izika kwa vitawi vyembamba. Jike hutaga mayai 2-4.
- Anabathmis hartlaubii, Chozi wa Principe (Principe Sunbird)
- Anabathmis newtonii, Chozi Mdogo wa Sao Tome (Newton's Sunbird)
- Anabathmis reichenbachii, Chozi wa Reichenbach (Reichenbach's Sunbird)
- Anthobaphes violacea, Chozi Kidari-machungwa (Orange-breasted Sunbird)
- Anthreptes anchietae, Chozi wa Anchieta (Anchieta's Sunbird)
- Anthreptes aurantius, Chozi Mkia-zambarau (Violet-tailed Sunbird)
- Anthreptes gabonicus, Chozi Kahawia (Mouse-brown Sunbird)
- Anthreptes longuemarei, Chozi Mgongo-zambarau (Western Violet-backed Sunbird)
- Anthreptes neglectus, Chozi wa Uluguru (Uluguru Violet-backed Sunbird)
- Anthreptes orientalis, Chozi kiuno-buluu (Eastern Violet-backed Sunbird)
- Anthreptes rectirostris, Chozi Kijani (Grey-chinned au Green Sunbird)
- Anthreptes reichenowi, Chozi Koo-buluu (Plain-backed Sunbird)
- Anthreptes rubritorques, Chozi Baka (Banded Green Sunbird)
- Anthreptes seimundi, Chozi Kijani Mdogo (Little Green Sunbird)
- Chalcomitra adelberti, Neli Koo-njano (Buff-throated Sunbird)
- Chalcomitra amethystina, Neli Mweusi (Amethyst Sunbird)
- Chalcomitra balfouri, Neli wa Sokotra (Socotra Sunbird)
- Chalcomitra fuliginosa, Neli Kahawiachekundu (Carmelite Sunbird)
- Chalcomitra hunteri, Neli Kidari-chekundu (Hunter's Sunbird)
- Chalcomitra rubescens, Neli Koo-kijani (Green-throated Sunbird)
- Chalcomitra senegalensis, Neli Gunda (Scarlet-chested Sunbird)
- Chalcomitra sp. nov., Neli wa Toha (Toha Sunbird)
- Cinnyris abbotti, Chozi wa Aldabra (Abbott's Sunbird)
- Cinnyris afer, Chozi Mkufu-mwekundu Mkubwa (Greater Double-collared Sunbird)
- Cinnyris batesi, Chozi wa Bates (Bates's Sunbird)
- Cinnyris bifasciatus, Chozi Mkufu-zambarau (Purple-banded Sunbird)
- Cinnyris bouvieri, Chozi Mabaka-machungwa Kusi (Orange-tufted Sunbird)
- Cinnyris chalcomelas, Chozi Kidari-zambarau (Violet-breasted Sunbird)
- Cinnyris chalybeus, Chozi Mkufu-mwekundu Mdogo Southern Double-collared Sunbird)
- Cinnyris chloropygius, Chozi Tumbo-zeituni (Olive-bellied Sunbird)
- Cinnyris coccinigaster, Chozi Mrembo (Splendid Sunbird)
- Cinnyris comorensis, Chozi wa Nzwani (Anjouan Sunbird)
- Cinnyris congensis, Chozi wa Kongo Congo Sunbird)
- Cinnyris coquerellii, Chozi wa Mayotte (Mayotte Sunbird)
- Cinnyris cupreus, Chozi Shaba (Copper Sunbird)
- Cinnyris dussumieri, Chozi wa Shelisheli (Seychelles Sunbird)
- Cinnyris erythrocercus, Chozi Kidari-chekundu (Red-chested Sunbird)
- Cinnyris fuelleborni, Chozi wa Fülleborn (Forest Double-collared Sunbird)
- Cinnyris fuscus, Chozi Kijivucheusi (Dusky Sunbird)
- Cinnyris habessinicus, Chozi Habeshi (Shining Sunbird)
- Cinnyris hofmanni, Chozi wa Hofmann (Hofmann's Sunbird)
- Cinnyris humbloti, Chozi wa Komori (Humblot's Sunbird)
- Cinnyris johannae, Chozi wa Johanna (Johanna's Sunbird)
- Cinnyris loveridgei, Chozi wa Loveridge (Loveridge's Sunbird)
- Cinnyris ludovicensis, Chozi-milima Ludwig's au Montane Double-collared Sunbird) – pengine inaainishwa katika C. afer
- Cinnyris manoensis, Chozi-miyombo (Miombo Double-collared Sunbird)
- Cinnyris mariquensis, Chozi wa Mariko (Marico Sunbird)
- Cinnyris mediocris, Chozi Mikufu-miwili (Eastern Double-collared Sunbird)
- Cinnyris minullus, Chozi Kibete (Tiny Sunbird)
- Cinnyris moreaui, Chozi wa Moreau (Moreau's Sunbird)
- Cinnyris nectarinioides, Chozi Tumbo-jeusi (Black-bellied Sunbird)
- Cinnyris neergaardi, Chozi wa Neergaard (Neergaard's Sunbird)
- Cinnyris notatus, Chozi Domo-refu (Malagasy Green au Madagascar Sunbird)
- Cinnyris oseus, Chozi Mabaka-machungwa Kaskazi (Palestine Sunbird)
- Cinnyris oustaleti, Chozi wa Angola (Oustalet's Sunbird)
- Cinnyris pembae, Chozi wa Pemba (Pemba Sunbird)
- Cinnyris prigoginei, Chozi wa Prigogine (Prigogine's Double-collared Sunbird) – pengine inaainishwa katika C. afer
- Cinnyris pulchellus, Chozi Mzuri (Beautiful Sunbird)
- Cinnyris regius, Chozi Mfalme (Regal Sunbird)
- Cinnyris reichenowi, Chozi Mikufu-miwili Kaskazi (Northern Double-collared Sunbird)
- Cinnyris rockefelleri, Chozi wa Rockefeller (Rockefeller's Sunbird)
- Cinnyris rufipennis, Chozi Mabawa-mekundu (Rufous-winged Sunbird)
- Cinnyris shelleyi, Chozi wa Shelley (Shelley's Sunbird)
- Cinnyris sovimanga, Chozi Mlambochi (Souimanga Sunbird)
- Cinnyris stuhlmanni, Chozi wa Stuhlmann (Ruwenzori Double-collared au Stuhlmann's Sunbird]]) – pengine inaainishwa katika C. afer
- Cinnyris superbus, Chozi Maridadi (Superb Sunbird)
- Cinnyris talatala, Chozi Tumbo-jeupe (White-bellied Sunbird)
- Cinnyris tsavoensis, Chozi wa Tsavo (Tsavo Sunbird) – pengine inaainishwa katika C. bifasciatus
- Cinnyris ursulae, Chozi wa Ursula (Ursula's Sunbird)
- Cinnyris usambaricus, Chozi wa Usambara (Usambara Double-collared Sunbird)
- Cinnyris venustus, Chozi Tumbo-njano (Variable Sunbird)
- Cyanomitra alinae, Neli Kichwa-buluu (Blue-headed Sunbird)
- Cyanomitra bannermani, Neli wa Bannerman (Bannerman's Sunbird)
- Cyanomitra cyanolaema, Neli Koo-buluu (Blue-throated Brown Sunbird)
- Cyanomitra obscura, Neli Zeituni Magharibi (Western Olive Sunbird) - labda ni spishi moja na C. olivacea
- Cyanomitra olivacea, Neli Zeituni Mashariki (Eastern Olive Sunbird)
- Cyanomitra oritis, Neli wa Kameruni (Cameroon Sunbird)
- Cyanomitra veroxii, Neli Kijivu (Grey au Mouse-coloured Sunbird)
- Cyanomitra verticalis, Neli Kichwa-kijani (Green-headed Sunbird)
- Deleornis axillaris, Chozi Kichwa-kijivu (Grey-headed Sunbird) – pengine inaainishwa katika D. fraseri
- Deleornis fraseri, Chozi Mabaka-mekundu (Fraser's au Scarlet-tufted Sunbird)
- Drepanorhynchus reichenowi, Neli Mabawa-dhahabu (Golden-winged Sunbird)
- Dreptes thomensis, Chozi Mkubwa wa Sao Tome (Giant au Sao Tome Sunbird)
- Hedydipna collaris, Chozi Mkufu (Collared Sunbird)
- Hedydipna metallica, Chozi wa Naili (Nile Valley Sunbird)
- Hedydipna pallidigaster, Chozi-pwani (Amani Sunbird)
- Hedydipna platura, Chozi Mdogo (Pygmy Sunbird)
- Nectarinia bocagii, Neli wa Bocage (Bocage's Sunbird)
- Nectarinia famosa, Neli Kijani (Malachite Sunbird)
- Nectarinia johnstoni, Neli Mabaka-mekundu (Scarlet- au Red-tufted Sunbird)
- Nectarinia kilimensis, Neli Shaba (Bronzy Sunbird)
- Nectarinia purpureiventris, Neli Kidari-zambarau (Purple-breasted Sunbird)
- Nectarinia tacazze, Neli Yakuti (Tacazze Sunbird)
Chozi kidari-machungwa
Chozi wa Anchieta
Chozi kahawia
Chozi mgongo-zambarau
Chozi kiuno-buluu
Chozi koo-buluu
Neli koo-njano
Neli mweusi
Neli kidari-chekundu
Neli koo-kijani
Neli gunda
Chozi mkufu-mwekundu mkubwa
Chozi mkufu-zambarau
Chozi mabaka-machungwa kusi
Chozi mkufu-mwekundu mdogo
Chozi tumbo-zeituni
Chozi mrembo
Dume la chozi shaba
Jike la chozi shaba
Chozi wa Shelisheli
Chozi kidari-chekundu
Chozi kijivucheusi
Chozi Habeshi
Chozi wa Mariko
Chozi mikufu-miwili
Chzoi kibete
Chozi tumbo-jeusi
Chozi domo-refu
Chozi mabaka-machungwa kaskazi
Chozi wa Pemba
Chozi mikufu-miwili kaskazi
Chozi mzuri
Chozi mfalme
Chozi wa Shelley
Chozi mlambochi
Chozi maridadi
Chozi tumbo-jeupe
Chozi tumbo-njano
Neli kichwa-buluu
Neli koo-buluu
Neli zeituni mashariki
Chozi kijivu
Neli kichwa-kijani
Chozi mabawa-dhahabu
Chozi mkufu
Chozi wa Naili
Chozi mdogo
Neli wa Bocage
Neli kijani
Neli mabaka-mekundu
Neli shaba
Neli kidari-zambarau
Neli yakuti
Handsome sunbird
Mount Apo sunbird
Fork-tailed sunbird
White-flanked sunbird
Green-tailed sunbird
Black-throated sunbird
Crimson sunbird
Brown-throated sunbird
Spectacled spiderhunter
Little spiderhunter
Streaked spiderhunter
Purple sunbird
Olive-backed sunbird
Long-billed sunbird
Crimson-backed sunbird
Purple-throated sunbird
Purple-rumped sunbird