Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani
Ligi ya mpira wa kikapu ya kulipwa ya Marekani Kaskazini From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Remove ads
Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (kwa Kiingereza: National Basketball Association au kifupi NBA) ni chama cha kitaifa cha timu za mpira wa kikapu zinazocheza katika ligi kuu huko Amerika ya Kaskazini ikijumuisha timu 29 toka Marekani na timu 1 toka Kanada. Ni moja ya ligi kubwa za kulipwa za mpira wa kikapu nchini Marekani na Kanada na ni ligi kubwa kabisa ya mpira wa kikapu duniani.

Ligi hii ilianzishwa huko New York City Juni 6, 1946 ikiwa na timu 11, ikiitwa Chama cha Mpira wa Kikapu Amerika (BAA). Ilichukua jina lake la sasa Agosti 3, 1949 baada ya kuungana na mshindani wake Ligi ya Kitaifa ya Mpira wa Kikapu National Basketball League (NBL).
Msimu wa ligi hii huanza Oktoba na kumalizika Aprili, kila timu ikicheza michezo 82. Wachezaji wa ligi hii ni wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa duniani kwa kutazama wastani wa mshahara kwa mwaka.[1][2]
Chama hiki ni mwanachama wa USA Basketball (USAB),[3] chama kinachotambuliwa na [Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu]] (the International Basketball Federation - FIBA). Makao yake makuu yako Midtown Manhattan, wakati studio za NBA Entertainment na NBA TV ziko Secaucus, New Jersey.
Orodha ya timu za ukanda wa Mashariki (kwa Kiingereza: "Eastern Conference"):
- Atlanta Hawks
- Boston Celtics
- Charlotte Hornets
- Chicago Bulls
- Cleveland Cavaliers
- Detroit Pistons
- Indiana Pacers
- Miami Heat
- Milwaukee Bucks
- New Jersey Nets
- New York Knicks
- Orlando Magic
- Philadelphia 76ers
- Toronto Raptors
- Washington Wizards
Orodha ya timu za ukanda wa Magharibi (kwa Kiingereza: "Western Conference"):
Remove ads
Marejeo
Soma zaidi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads