From Wikipedia, the free encyclopedia
Chake Chake ni mji mkubwa kwenye kisiwa cha Pemba ambacho ni sehemu ya Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ni makao makuu ya wilaya ya Chake Chake katika mkoa wa Pemba Kusini (South Pemba).
Chake Chake | |
Mahali pa mji wa Chake Chake katika Tanzania |
|
Majiranukta: 5°14′24″S 39°46′12″E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Pemba Kusini |
Wilaya | Chake Chake |
Katika kata tatu za Chachani, Tibirinzi na Wara kuna takriban wakazi 15,000.
Mji umeenea kwenye kilima juu ya hori inayoingia ndani ya kisiwa. Bandari ya Chake Chake haina kina cha kutosha kwa meli hivyo hutumiwa na jahazi au dau ndogo tu.
Kitovu cha mji ni eneo la sokoni penye maduka, hospitali, boma la kale na hoteli ya SMZ. Kando la mji kuna uwanja mpya wa michezo na hospitali mpya.
Uwanja wa ndege wa Wawi uko kilomita saba kutoka mjini upande wa mashariki. Huo ni uwanja wa ndege wa pekee kisiwani ukihudumia ndege ndogo tu.
Kulikuwa mahali pa makazi ya Waswahili wa kale, lakini hakuna majengo ya kihistoria inayoonekana ila tu boma la kale. Habari zake zimepatikana tangu karne ya 19.
Wataalamu huamini ya kwamba umeanzishwa tayari na Wareno karne 4 - 5 zilizopita kwa sababu minara yake yenye umbo la mraba si kawaida katika ujenzi wa Waswahili na Waarabu.
Chini ya mji kuelekea kihori kuna bado mabaki ya boma dogo lenye mizinga miwili ya kale.
Makala hii kuhusu maeneo ya Pemba bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Chake Chake kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.