From Wikipedia, the free encyclopedia
Biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki ni jina la kutaja aina ya biashara iliyokuwa ikifanyika kutoka katika pwani hadi ndanindani ya Afrika Mashariki. Awali ilianza katika maeneo ya pwani ya Afrika Mashariki na kisha kuenea katika vijieneo vya ndani kabisa vya Afrika Mashariki.
Biashara hii inasemekana ilianzia karne ya 18 na 19, ikachukua zaidi ya miaka 30-50 hadi ilipokuja kuingiliwa na wakoloni mwishoni kabisa mwa karne ya 19.
Wafanyabiashara wakuu waliohusishwa na biashara hiyo walikuwa Waarabu na Waswahili kutoka Pwani na Wayao kutoka kusini mwa Tanganyika, Wakamba kutoka kusini mwa Kenya na vilevile Wanyamwezi kutoka Tabora. Makabila mengi yalishiriki katika biashara hiyo, lakini vingunge wenyewe ni Wayao, Wakamba na Wanyamwezi.
Biashara ilikuwa katika muundo wa misafara mitatu ambayo ilianzia pwani ikaenda hadi ndanindani kabisa mwa ukanda wa Afrika Mashariki. Misafara hiyo ilikuwa kama ifuatavyo:
Safari ilianzia Mombasa na baadhi ya maeneo ya Pangani hadi maeneo ya Kilimanjaro kuelekea pembezoni mwa ziwa Victoria, kupitia Wakikuyu, Wataita, Wamaasai, na Wanyika. Msafara huo ulikuwa unaongozwa na Wakamba kutoka Kenya.
Msafara huu ulianzia Bagamoyo kupitia maeneo ya kati ya Tanganyika - Tabora (Unyanyembe). Kuanzia huko msafara ulienda hadi Ujiji, halafu Buganda kupitia Buhaya, magharibi mwa fukwe ya Ziwa Victoria. Msafara ulikuwa chini ya Wanyamwezi ambao katika karne ya 19 walikuwa chini ya Mtemi Mirambo na Mtemi Nyungu ya Mawe na Mtemi Fundikira mnamo 1839. Msafara huu ulikuwa una shughuli nyingi na muhimu sana kupita misafara yote mitatu.
Msafara huu ulianzia katika bandari ya Mikindani na Kilwa kuelekea kanda ya Ziwa Tanganyika kupitia kusini mwa Ziwa Nyasa. Msafara ulifika Monomutapa kwa ajili ya dhahabu. Ulikuwa chini ya Wayao ambao walikuwa chini ya Mataka I kwenye karne ya 19. Wayao walifanya biashara kaskazini mwa Kilwa na Zambezi ya chini kuelekea Kusini. Baadaye walipata silaha wakawa viongozi mara moja katika maeneo ya Ziwa Nyasa na pwani. Wayao walishikiri msafara wa Kusini ambao uliishia Afrika ya Kati wakati Wakamba walikuwa Kaskazini na Wanyamwezi walishikiria msafara wa Kati ulioanzia Bagamoyo hadi Ujiji.
Wafanyabiashara wa Waswahili na Waarabu kutoka pwani waliuza bunduki, shanga, unga wa bunduki, nguo na bidhaa nyingine za kiwandani. Watu kutoka ndanindani kabisa mwa Afrika Mashariki walitoa bidhaa kama vile pembe za ndovu, nta ya nyuki, dhahabu, ngozi za wanyama na vitu vingine vya thamani.
Kuibuka na kuendelea kwa biashara ya masafa marefu ya Afrika Mashariki kulichangiwa na mambo kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na:
Hili lilitokana na kuongezeka kwa uzalishaji hasa katika sekta ya kilimo.
Kuibuka kwa jamii kubwa ya wafanyabiashara katika Afrika Mashariki kama vile Wanyamwezi, Wayao na Wakamba nako kulichangia kukua kwa biashara.
Uwepo wa miji mikubwa ya pwani kama vile Bagamoyo, Mikindani na Pangani kuliongezea ukuaji wa biashara kwa kufuatia wa kwamba miji hiyo ilikuwa kianzio cha safari za masafa marefu wakati wa uendeshaji wa biashara.
Biashara ya masafa marefu ilikuwa na matokeo kadha wa kadha katika maeneo ya pwani hadi ndanindani kabisa mwa Afrika Mashariki. Matokeo hayo ni pamoja na:
Biashara ilipelekea kukua kwa miji na vijiji hasa ndanindani huko mwa Afrika Mashariki kwa mfano Ujiji, Mpwapwa, Tabora na kwingineko.
Biashara hii ilichangia kiasi kikubwa kukua kwa dola mbalimbali za kitemi kama vile Wanyamwezi, Ukimbu, na Wahehe katika maeneo ya Tanganyika. Vilevile dola la Buganda lilikuja kukua mno katika karne ya 19 kwa kufuatia biashara hii.
Tamaduni mpya, kwa mfano dini ya Kiislamu na mtindo wa uvaaji wa kanzu na baraghashia ulienea ndani kabisa ya Afrika Mashariki.
Lugha ya Kiswahili ilienea kwa kiasi kikubwa sana kutoka katika pwani ya Afrika Mashariki hadi maeneo ya ndani kwa sababu wafanyabiashara walikuwa wanatumia Kiswahili kama chombo cha mawasiliano wakati wa kubadilishana bidhaa.
Biashara ya masafa marefu ilienda sambamba na ukuaji wa biashara ya utumwa - hasa katika maeneo ya ndani ya Afrika Mashariki.
Kuna baadhi ya watu walioibuka kama wafanyabiashara na viongozi wakubwa nje ya biashara kwa kufuatia utajiri uliokithiri kutoka katika biashara. Hili lilijumlisha Mirambo, Machemba, [Nyungu ya Mawe]] na Mkwawa.
Watu kutoka maeneo ya pwani walioana au kuzaliana na watu kutoka ndani kabisa mwa Afrika Mashariki.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.