From Wikipedia, the free encyclopedia
Ibuti la Jauza (jina la kisayansi Alpha Orionis, kwa Kiingereza Betelgeuse) ni nyota ya aina ya jitu jekundu inayoonekana katika kundinyota Jabari (Orion).
Jina la Ibuti la Jauza lilijulikana tangu karne nyingi kati ya mabaharia Waswahili waliotumia nyota hii kama msaada wa kukuta njia yao baharini wakati wa usiku. Asili ya jina ni Kiarabu إبط الجوزاء (ibt al jauza) . Ibuti inamaanisha "kwapa" na Jauza ni ni jina la zamani kwa Jabari, kwa maana ya "katikati" maana kuna majira ambako nyota hizo ziko katikati kwenye anga. Jina la Kirabu lilipokewa pia na wanaastronomia wa Ulaya wakati wa karne za kati na kwa matamshi ya kigeni kutoka "i-bt-al-geusa" kuwa "Bet-el-geuse". [1]
Jina la kitaalamu la kisasa ni "Alpha Orionis" (α Orionis) kwa sababu ilionekana kuwa nyota angavu zaidi katika kundiyota yake.[2]. "Betelgeuse" ilikubaliwa na kuthibitishwa na UKIA kuwa jina maalum.[3].
Ni nyota angavu ya tisa kati ya nyota zote zinazoonekana angani na nyota angavu ya pili kwenye Sayadi (Orion). Uangavu wake unachezacheza kati ya vipimo vya 0.2 na 1.2.[4]
Umbali wake na dunia ulikadiriwa mnamo mwaka 2008 kuwa miakanuru 640[5]
Umri wa Ibuti la Jauza haukutimiza miaka milioni 10 lakini umeendelea haraka kutokana na masi yake kubwa. [6]
Ibuti la Jauza imeshaendelea kufikia ngazi za mwisho za mageuzi ya nyota (stellar evolution). Katika kipindi cha miaka milioni 1 ijayo inakadiriwa kutimiza mageuzi yake hadi kulipuka kama nyota nova. [7]
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.