Jabari ni kundinyota linalojulikana pia kwa jina lake la kimagharibi la Orion. Ni moja ya makundinyota yanayotambuliwa na Umoja wa Kimataifa wa Astronomia [1]

Thumb
Jabari - Orion
Thumb
Nyota za Jabari jinsi zinavyoonekana; juu kushoto iko Ibuti la Jauza (Betelgeuse), chini kulia Rijili ya Jabari (Rigel) na chini katikati Nebula ya Jabari (Orion nebula)

Nyota za Jabari huwa hazipo pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisia kuna umbali mkubwa kati yake, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Jabari" linaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoliona kutoka duniani.

Jina

Jina la Kiswahili ni Jabari na linatokana na Kiarabu الجبار al-jabbaar ambalo linamaanisha "jitu". Jina hili lilipokewa na Waarabu kutoka kwa Waaramu waliosema gabbara "jitu"[2]. Wote walimaanisha hapa tabia ya mwindaji mkuu na nusu-mungu katika mitholojia ya Kigiriki aliyeitwa Ὠρίων orion na hivyo alitajwa katika kitabu cha Almagesti cha Klaudio Ptolemaio.

Nyota

Jabari ni kati ya makundinyota yanayoonekana vyema kwenye angakusi na pia angakaskazi ya Dunia. Nyota saba angavu sana zinakumbukwa kirahisi na watazamaji wa anga.

Nyota nne za Rijili ya Jabari (Rigel), Ibuti la Jauza (Betelgeuse), Bellatrix and Saiph zinafanya pembenne, na katikati kuna safu ya nyota tatu za karibu zinazoitwa "ukanda" ambazo ni Alnitak, Alnilam na Mintaka (ζ, ε na δ Orionis). Chini ya nyota za ukanda kuna nyota angavu inayotambuliwa kwa darubini ndogo kuwa nebula angavu, hii ni Nebula ya Jabari (Orion nebula).

Maelezo zaidi Jina la (Bayer), Namba ya Flamsteed ...
Jina la
(Bayer)
Namba ya
Flamsteed
Jina
(UKIA)
Mwangaza
unaoonekana
Umbali
(miakanuru)
Aina ya spektra
α 58 Ibuti la Jauza - Betelgeuse 0,0 bis 1,3m 640 M1-2Ia-Iab
β 19 Rijili ya Jabari - Rigel 0,03 bis 0,3m 773 B8Iab + B9V + B9V
γ 24 Bellatrix 1,64m 243 B2III
ε 46 Alnilam 1,69m 1342 B0Iab
ζ 50 Alnitak 1,74m 818 O9.7Ibe + O + B0III
κ 53 Saiph 2,07m 722 B0.5Iavar
δ 34 Mintaka 2,20 bis 2,35m 916 O9.5II + B2V
ι 44 Hatysa 2,75m 1326 O9III
π3 1 Tabit 3,19m 26 F6V
Funga

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya Nje