From Wikipedia, the free encyclopedia
Kwa maana tofauti wa jina hili angalia kondoo. Kwa maana tofauti ya Hamali angalia hapa Mpagazi
Kondoo (pia: Punda, zamani Hamali, Aries) ni kundinyota ya zodiaki linalojulikana pia kwa jina lake la kimagharibi la Aries[1]. Hamali pia ni jina la kimataifa kwa nyota angavu zaidi kati kundinyota hili.
Nyota za Kondoo huwa haziko pamoja kihalisi lakini zinaonekana tu vile kutoka duniani. Kwa uhalisi kuna umbali mkubwa kati yao, kama ziko mbali au jirani nasi. Kwa hiyo kundinyota "Kondoo" inaonyesha eneo la angani jinsi tunavyoiona kutoka Duniani.
Kondoo ni tafsiri ya Hamali. Mabaharia Waswahili walijua nyota hizi tangu muda mrefu kwa jina la "Hamali".[2]
Hamali linatokana na Kiarabu حمل ḥamal ambalo linamaanisha "kondoo". Jina hili lilipokelewa na Waarabu kutoka kwa Wagiriki wa Kale waliosema Κριός krios "dume wa kondoo" na hao walipokea tayari (kundinyota)| hii kutoka Babeli. [3] [4]
Katika unajimu wa kisasa katika Afrika ya Mashariki jina "Hamali" limesahauliwa ikiwa kundinyota linatafsiriwa tu "Kondoo".
Kondoo iko angani kwenye mstari wa Zodiaki kati ya Samaki (pia Hutu, lat. Pisces) na Ng'ombe (pia Tauri, lat. Taurus) .
Kondoo huwa na nyota angavu 3 hasa zilizotumiwa kwa ubaharia tangu zamani.[5] Hizi mara nyingi zinatajwa kama Alpha, Beta na Gamma Arietis [6].
Alpha Arietis inajulikana kimataifa pia kwa jina la "Hamali" kwa sababu majina mengine ya Kiarabu yaliyopokelewa na wanaastronomia wa Ulaya. Ni nyota jitu yenye rangi ya kichungwa na mwangaza unaoonekana wa mag 2.0. Umbali wake na dunia ni mwakanuru 66 na uangavu haĺisi ni −0.1.
Beta Arietis inayoitwa pia Sheratan ina rangi ya buluu-nyeupe na mwangaza unaoonekana wa 2.64 ikiwa umbali wa miakanuru 59 kutoka Dunia.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.