Baraza la mawaziri Tanzania 2015
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Baraza la Mawaziri la Tanzania ni ngazi ya juu ya serikali au mkono wa utendaji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mfumo wa mgawanyo wa madaraka.
Baraza hili linaundwa na rais, makamu wa rais, rais wa Zanzibar, waziri mkuu na mawaziri wote. [1] Manaibu mawaziri si sehemu ya baraza. Mwanasheria Mkuu anashiriki katika mikutano ya baraza lakini hana haki ya kupiga kura katika mikutano hiyo.
Mikutano ya baraza huongozwa na Rais kama mwenyekiti, kama Rais hayupo basi mikutano hiyo huongozwa na Makamu wa Rais, na kama wote wawili hawapo mikutano hiyo huongozwa na Waziri Mkuu.[2]
Serikali iliyotangazwa na John Magufuli, rais wa tano wa Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015 mnamo tarehe 10 Desemba 2015. Isipokuwa nafasi 4 zilichelewa kutajwa majina hadi tarehe 23 Desemba, na hapo waliingia Jumanne Maghembe, Philip Mpango, Gerson Lwenge na Joyce Ndalichako. Siku hiyohiyo Makame Mbarawa alihamishwa kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kwenda Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Chama anachotoka | Chama Cha Mapinduzi |
---|
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.