Bahari ya Beaufort
From Wikipedia, the free encyclopedia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Bahari ya Beaufort ni bahari ya pembeni ya Bahari Aktiki[1].
Iko upande wa kaskazini wa pwani za Alaska (Marekani) na majimbo ya Yukon na Kaskazini-Magharibi ya Kanada.
Upande wa magharibi inakutana na Bahari ya Chukchi, upande wa mashariki inapakana na visiwa vya Aktiki vya Kanada.
Jina lake lilichaguliwa kwa heshima ya Francis Beaufort (1774–1857) aliyekuwa mtaalamu wa ramani za bahari katika jeshi la majini la Uingereza wakati wa karne ya 19.
Sehemu hii ya bahari ina eneo la kilomita za mraba 476,000 na kina chake inafikia hadi mita 4,683, kina cha wastani ni mnamo mita 1,000. Chini ya bahari kuna akiba za mafuta na gesi.
Bahari imefunikwa na barafu sehemu kubwa ya mwaka. Kuna nyangumi wengi aina ya Beluga. [2].
Eneo lenye umbo la pembetatu kwenye mpaka wa Marekani na Kanada linadaiwa na nchi zote mbili, umuhimu wake uko katika swali la haki ya kuamulia matumizi ya malighafi hizi.
Mto mkubwa unaopeleka maji yake baharini ni mto Mackenzie wa Kanada.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.