From Wikipedia, the free encyclopedia
Baekje au Paekche (Tamka pɛk̚tɕe) (18 KK – 660 KE) ulikuwa ufalme uliopo mjini kusini-magharibi mwa nchi ya Korea. Hii ilikuwa moja kati ya Falme Tatu za Korea, pamoja na Goguryeo na Silla.
Ufalme wa Korea Baekje |
---|
|
Baekje ilianzishwa na Onjo, mtoto wa tatu wa mwanzilishi wa Goguryeo Jumong na So Seo-no, mjini Wirye-sung (Seoul ya leo). Baekje, kama jinsi ilivyo Goguryeo, alidai kuuchukua Buyeo, nchi ilioanzishwa katika Manchuria ya leo kunako kipindi cha kuanguka kwa Gojoseon.
Baekje imepata mapigano tofauti na kuamua kuungana na Goguryeo na Silla wakiwa kama falme tatu zilizoweza kueneza kudhitibi peninsula. Kwenye kilele chake cha karne ya nne, Baekje imeweza kudhitibi baadhi ya kolono huko Uchina na sehemu kubwa ya magharibi mwa Peninsula ya Korea, na vilevile Pyongyang. Ikaja kuwa na nguvu sana kwa upande wa kanda ya bahari, kwa uhusiano wa kisiasa na kibiasha na Uchina na Japani.
Mnamo mwaka wa 660, ikajakuangushwa na nguvu ya muungano baina ya Silla na Nasaba ya Tang ya Uchina, ikajisalimisha kwa Muungano wa Silla.
Wakati wa utawala wa Mfalme Goi (234–286), Baekje ikawa imejiendeleza kabisa ufalme wake, kama jinsi ilivyoendelea kuleta makubaliano mazuri ya Mahan. Mnamo 249, kulingana na maandishi ya kale ya Kijapani ya Nihonshoki, uenezi wa Baekje ulifika hadi mashariki mwa Gaya, maeneo ya bonde la Mto Nakdong. Baekje ilielezewa kwa mara ya kwanza kama ufalme kwenye rekodi za Kichina mnamo 345. Mpango wa kwanza wa kiplomasia kutoka Baekje ulifikia hadi huko nchini Japani kunako 367 (kwa mujibu wa Nihon Shoki : 247).
Mfalme Geunchogo (346–375) alipanua maeneo ya Baekje kwa upande wa kaskazini kwa kupitia vita dhidi ya Goguryeo, wakati anaanza kuchukua mamlaka ya jamii za Mahan zilizobakia huko mjini kusini. Wakati wa utawala wa Geunchogo, maeneo ya Baekje yalikuwemo upande zaidi ya magharibi mwa Peninsula ya Korea (kasoro mikoa miwili tu ya Pyeongan), na mnamo 371, Baekje ikashindwa na Goguryeo huko Pyongyang. Baekje ikaendelea kufanya shughuli za kiabiashara na Goguryeo, na kupelekea kuchukua tamaduni za Kichina na teknolojia. Ubudha ukawa dini rasmi ya kwanza nchini mnamo 384.
Baekje ikawa ina nguvu kwa upande bahari na kuendeleza mahusiano mazuri ya kihisani na viongozi wa Kijapani wakati wa Kipindi cha Kofun, ikabadilisha athira za kitamaduni kibara huko Japani. Mfumo wa uandikaji wa Kichina, Ubudha, uliendelea siku hadi siku, sherehe za mazishi, na mambo mengine ya kitamaduni yalianzishwa na wakubwa, mafundi, wasomi, na mamonki kwa kupitia mahusiano yao mazuri.[1]
Wakati wa kipindi hicho, beseni la Mto Han limebaki kama ardhi-moyo wa nchi.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.