Gojoseon (고조선, 古朝鮮) ulikuwa ufalme wa kale wa Korea. Ufalme huu hehasabiwa kama taifa sahihi kabisa la watu wa Korea. Kwa mujibu wa Samguk Yusa na rekodi nyingine za zama za kati za Kikorea,[1] Gojoseon inasemekana kwamba ilianzishwa mnamo 2333 KK na mkongwe Dangun, ambaye anasemekana kwamba anatokea kwenye Ukoo wa Mbinguni (天孫, 천손). Ilikuwa katikati ya beseni la Mto Liao na upande wa kaskazini mwa Peninsula ya Korea.

Thumb
Gojoseon

Watu wa Gojoseon

Watu wa Gojoseon waliishi huko kaskazini-mashariki mwa Manchuria ya kale na hutazamiwa kama ndugu wa kwanza kunadikwa kwenye rekodi za Korea.[2] Watu wa Gojoseon walikuwa wakirekodiwa kwenye maandiko kadhaa ya Kichina wakiwa kama moja kati ya Dongyi, maana yake "washenzi wa mashariki".

Watu wa Gojoseon walikuwa vizazi vya kabila la wahamiaji wa Altaic waliolewea huko Manchuria, mashariki ya mbali ya Uchina, na Peninsula ya Korea. Gojoseon hatimaye wakajikita kwenye eneo dogo la Manchuria na Peninsula ya Korea.

Eneo

Awali, Gojoseon huenda ilikuwa mjini Liaoning; lakini kunako 400 KK, ikahamia karibu na Pyongyang, mji mkuu wa sasa wa Korea Kaskazini.[3][4]

Tazama pia

  • Historia ya Korea
  • Samjoseon

Marejeo

Wikiwand in your browser!

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.

Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.