From Wikipedia, the free encyclopedia
Al-Haji Sir Ahmadu Bello (12 Juni 1910 - 15 Januari 1966) alikuwa mwanasiasa nchini Nigeria, na alikuwa Waziri wa kwanza kutoka mkoa wa Kaskazini mwa Nigeria miaka 1954-1966.
Ahmadu Bello | |
Premier of Northern Nigeria | |
---|---|
Muda wa Utawala 1954 – 1966 | |
aliyemfuata | Hassan Katsina |
tarehe ya kuzaliwa | 12 Juni 1910 Rabbah, Sokoto State. |
tarehe ya kufa | 14 Januari 1966 |
chama | Northern People's Congress |
dini | Muslim |
Alikuwa mmoja wa viongozi maarufu Kaskazini mwa Nigeria sambamba na Abubakar Tafawa Balewa, wote wawili maarufu katika mazungumzo kuhusu nafasi ya kanda hili katika Nigeria huru. Kama kiongozi wa Northern People's Congress, chama hiki kiliweza kushinda uchaguzi wa ubunge mwaka wa 1959.
Hata hivyo, aliuawa tarehe 15 Januari 1966.
Yeye alizaliwa katika Rabbah, mjini Sokoto S akiwa mtoto wa mkuu wa wilaya na mrithi wa milki ya Sokoto. Babu-mkuu wake alikuwa Sultani Bello, mwanzilishi wa Sokoto na mwana wa mheshimiwa Usman Dan Fodio.
Ahmadu Bello alipata elimu yake ya kwanza katika Shule ya Mkoa wa Sokoto, shule ya kisasa pekee wakati huo katika jimbo la Sokoto. Kisha, aliendelea katika chuo cha Ualimu cha Katsina.
Baada ya miaka mitano huko, aliteuliwa na Sultani kuwa mwalimu katika shule ya kati ya Sokoto, shule yake ya zamani ambayo ilikuwa imebadilika.
Mwaka wa 1934, aliteuliwa mkuu wa Rabbah, miaka minne baadaye alitumwa Gusau kuwa mkuu wa tarafa. Mwaka wa 1938, alifanya jitihada kuwa Sultani wa Sokoto lakini aliambulia nunge. Aliyepata kiti cha Sultan alimteua Ahmadu Bello kama "Sarduna", mengine yameandikwa "Sardauna", na kumpatia mamlaka katika baraza la Sokoto.
Mwaka wa 1948, alipewa udhamini kujifunza utawala wa serikali za mitaa nchini Uingereza. Ahmadu Bello alichukua udhamini akigundua kuwa alihitaji kuendeleza maarifa yake kuhusu mchakato wa utawala.
Baada ya kurudi kutoka Uingereza, aliteuliwa kuwakilisha mkoa wa Sokoto katika Bunge la mikoa. Kama mwanachama wa baraza, alikuwa mashuhuri kwa maslahi ya kaskazini na kuvutiwa na mtindo wa mashauriano na makubaliano na wawakilishi wakuu ya emirati za kaskazini: Kano, Bornu na Sokoto.
Katika uchaguzi wa kwanza uliofanyika Kaskazini mwa Nigeria mwaka 1952, Bwana Ahmadu Bello alishinda [[kiti[[cha bunge cha Kaskazini, na kuwa mwanachama wa baraza tendaji kikanda kama waziri wa kazi. Bello aliweza kufanikiwa kuwa waziri wa Ujenzi, katika Serikali za Mitaa, na ya Ustawi wa Jamii katika Mkoa wa Kaskazini mwa Nigeria.
Mwaka wa 1954, Bello aliweza kuwa mkuu wa kwanza wa Kaskazini mwa Nigeria. Katika Uchaguzi mkuu huru wa mwaka wa 1959, Bello aliongoza NPC kushinda viti vingi vya bunge. Chama cha Bello NPC kiliungana na chama cha Nnamdi Azikiwe NCNC (Baraza la Taifa la Nigeria na Kamerun) na kuunda serikali ya kwanza ya shirikisho la Nigeria ambayo ilileta uhuru kutoka Uingereza. Katika kutengeneza shirikisho la serikali huru ya Nigeria mwaka wa 1960, Bello alichagua kubaki mkuu wa Kaskazini mwa Nigeria na kumwachia makamu wa rais wa NPC Abubakar Tafawa Balewa nafasi ya Waziri Mkuu wa Shirikisho hilo.
Tendo kuu la Bello na urithi mkubwa alioacha ni kuunganisha watu mbalimbali wa Kaskazini mwa Nigeria. Aliuawa wakati wa mapinduzi ya kijeshi baada ya kuangusha serikali huru nchini Nigeria tarehe 15 Januari 1966 alipokuwa anatumikia kama mkuu wa Kaskazini mwa Nigeria wakati huo.
Chuo Kikuu cha Ahmadu Bello kimerithi jina lake. Picha yake iko katika noti ya Nigeria ya naira 200.
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.