From Wikipedia, the free encyclopedia
Aaliyah Dana Haughton (16 Januari 1979 – 25 Agosti 2001) alikuwa msanii wa rekodi, mwigizaji, na mwanamitindo kutoka nchini Marekani. Alijulikana sana kwa jina la kisanii kama Aaliyah. Aaliyah alizaliwa mjini Brooklyn, New York, na kukulia mjini Detroit, Michigan. Wakati wa umri wake wa awali, amepata kuonekana kwenye kipindi cha televisheni cha Star Search na kutumbuiza kwenye onyesho hilo na Gladys Knight. Akiwa na umri wa miaka 12, Aaliyah aliingia mkataba na Jive Records na Blackground Records na mjomba wake, Barry Hankerson. Akamtambulisha kwa R. Kelly, ambaye baadaye akaja kuwa mshauri wake, vilevile mtunzi na mtayarishaji wake kiongozi wa albamu yake ya kwanza, Age Ain't Nothing But a Number. Albamu iliweza kuuza nakala milioni mbili kwa nchini Marekani na kutunukiwa platinamu mbili na Recording Industry Association of America (RIAA). Baada ya kukumbwa na mshtaka ya ndoa haramu na Kelly, Aaliyah akavunja mkataba wake na Jive na badala yake kuingia mkataba na studio ya Atlantic Records.
Aaliyah | |
---|---|
Aaliyah mnamo mwaka 2000. | |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Aaliyah Dana Haughton |
Amezaliwa | Brooklyn, New York City, New York, United States | Januari 16, 1979
Asili yake | Detroit, Michigan, United States |
Amekufa | Agosti 25, 2001 (umri 22) Marsh Harbour, Visiwa vya Abaco, The Bahamas |
Aina ya muziki | R&B, pop, hip hop |
Kazi yake | Mwimbaji, mnenguaji, mwigizaji, mwanamitindo |
Miaka ya kazi | 1991–2001 |
Studio | Blackground, Jive, Atlantic, Virgin, Universal |
Tovuti | www.aaliyah.com |
Aaliyah amefanya kazi na watayarishaji kama vile Timbaland na Missy Elliott kwa ajili ya albamu yake ya pili ya One in a Million; imeuza nakala milioni mbili kwa nchini Marekani na nakala zaidi ya milioni nane kwa hesabu ya dunia nzima. Mnamo mwaka wa 2000, Aaliyah amepata kuonekana kwenye filamu yake ya kwanza -liokwenda kwa jina la Romeo Must Die. Amechangia kibwagizo cha filamu hiyo, ambacho ni "Try Again". Wimbo ulishika nafasi ya juu kwenye chati za Billboard Hot 100 katika airplay pekee, inamfanya Aaliyah kuwa msanii wa kwanza kufaula hivi katika historia ya Billboard. "Try Again" imepata kushindinishwa kwenye Grammy Award kwa ajili Msanii Bora wa Kike wa R&B.
Albamu za Studio
|
Kompilesheni
|
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.