Zuzu
Edited by Aidan Mhalinga / From Wikipedia, the free encyclopedia
Zuzu ni kata ya Dodoma Mjini katika Mkoa wa Dodoma, Tanzania.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 10,054 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 6,485 [2] waishio humo.
Kata ya Zuzu ina jumla ya mitaa 5 ambayo ni Mtaa wa Mazengo, Mtaa wa Pinda, Mtaa wa Sokoine, Mtaa wa Chididimo na Mtaa wa Soweto.
Wakazi wa kata hii ni hasa wakulima na wafugaji pia ni wafanyabiashara.
Kata ina jumla ya shule 3 za msingi ambazo ni S/m Zuzu, S/m Chididimo na S/m Soweto ambayo ni mpya kwa sasa.
Pia kata ina shule moja ya sekondari ambayo ni Shule ya Sekondari Zuzu.