Ziwa Maracaibo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Ziwa Maracaibo (Kihispania: Lago de Maracaibo) ni eneo kubwa la maji nchini Venezuela karibu na Bahari ya Atlantiki. Limeunganishwa na Bahari Karibi kwa njia ya mfereji wenye upana wa km 5.5. Kupitia mfereji huo maji ya chumvi hungia ndani yake. Kwa upande mwingine ziwa linalishwa na mito mingi. Upande wa kaskazini maji yake huwa ya chumvi-chumvi, upande wa kusini huwa maji matamu. Hivyo lina tabia ya hori ya bahari lakini pia ya ziwa [1] [2] [3] [4]. Kwa kawaida huitwa "ziwa", si "hori"[5].
| |
Nchi zinazopakana | Venezuela |
Eneo la maji | km2 13,512 |
Kina cha chini | m 60 |
Kimo cha uso wa maji juu ya UB |
m 0 |
Miji mikubwa ufukoni | Maracaibo, Cabimas, Ciudad Ojeda |
Jina lake limetokana na mji wa Maracaibo, ambao upo upande wa mashariki mwa mfereji wa kuingia baharini. Pale Maracaibo mfereji huwa na upana wa km 8.5 ukivukwa kwa daraja refu. [6]
Ziwa Maracaibo huwa na vipimo vya km 160 kwa km 110. Idadi ya mito inayoishia humo ni 135 na mkubwa kati yake ni Mto Catatumbo.