![cover image](https://wikiwandv2-19431.kxcdn.com/_next/image?url=https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/18/Great-Zimbabwe.jpg/640px-Great-Zimbabwe.jpg&w=640&q=50)
Zimbabwe Kuu
From Wikipedia, the free encyclopedia
Zimbabwe Kuu (kwa Kiingereza: Great Zimbabwe ulikuwa mji wa Karne za Kati katika vilima vya kusini-mashariki mwa Zimbabwe karibu na Ziwa Mutirikwi na mji wa Masvingo. Inafikiriwa ulikuwa mji mkuu wa dola kubwa lisilojulikana sana.[1]
![Thumb image](http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/1/18/Great-Zimbabwe.jpg/640px-Great-Zimbabwe.jpg)
Majengo yake ya mawe ni ya kuanzia karne ya 9 hadi karne ya 15, mji ulipoachwa. Inasadikiwa kwamba wakazi bwake waliweza kufikia 18,000 na kuwa mababu wa Washona wa leo.[2]
Magofu yake yameorodheshwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia.