Yuda Mmakabayo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yuda Mmakabayo (kwa Kiebrania: יהודה המכבי,[1] Yehudah ha-Makabi) alikuwa kuhani wa Israeli, mwana wa tatu wa Matathia, aliyeongoza taifa lake dhidi ya Dola la Waseleuko (167–160 KK) ili kupata uhuru wa dini na hatimaye uhuru wa taifa upande wa siasa pia.[2].
Sikukuu ya Hanukkah ("Kutabaruku") ilianzishwa chini yake kufanya kila mwaka ukumbusho wa ushindi uliomwezesha kutakasa hekalu la Yerusalemu mwaka 164 KK.
Ukoo wake (Wahasmonei) uliendelea kutawala Yudea hadi 63 KK, wakisisitiza dini ya Uyahudi na kupunguza athari ya ustaarabu wa Ugiriki wa kale kati ya Wayahudi.