Yothamu wa Yuda
From Wikipedia, the free encyclopedia
Yothamu (kwa Kiebrania: יוֹתָם, Yōtam, Yōṯam, "Mungu ni mwadilifu"; kwa Kigiriki: Ιωαθαμ, Ioatham; kwa Kilatini: Joatham)[1] alikuwa mfalme wa Yuda kwa miaka 16, akimrithi baba yake Uzia wa Yuda (2 Fal 15:33 na 2 Nya 27:1) hadi alipoondolewa madarakani na wapinzani na hatimaye kurithiwa na mwanae Ahazi.
Wakati wake walifanya kazi manabii Amosi, Isaya na Mika.
Injili ya Mathayo inamtaja katika orodha ya vizazi vya Yesu.